Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amesema wako tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania ambao utapigwa kesho Jumatatu, Februari 10 katika uwanja wa Isamuhyo
Akizungumza katika Mkutano na wamahabari mapema leo, Hamdi alisema amepata nafasi ya kuifutilia JKT Tanzania, ni timu nzuri ambayo inapenda kucheza mpira hivyo anatarajia mchezo utakuwa mgumu
Hata hivyo Hamdi amesema Yanga ni timu bora na wanakwenda kwenye mchezo huo wakiwa na dhamira ya kusaka matokeo ya ushindi
"Tunatambua kuwa Kesho tutakuwa na mchezo mgumu lakini tutafanya juhudi kubwa kuhakikisha tunapata alama tatu"
"Namewaona JKT Tanzania ni timu nzuri na wanapenda kucheza vizuri hivyo sisi tutajiandaa kucheza vizuri ili kupata alama tatu,"alisema
Kocha huyo mwenye uraia pacha wa nchi za Algeria na Ufaransa amesisitiza kuwa hajali timu yake itafunga mabao mangapi katika mchezo huo. Jambo muhimu ni kuondoka na alama tatu
"Ni kweli mchezo uliyopita tumefunga magoli 6 na ni kwa sababu tuna kikosi bora, Jukumu letu ni kuhakikisha tunafanya vizuri kila mchezo"
"Nina imani kubwa kwa Wachezaji wangu na tumezungumza kuwa kwa sasa kitu muhimu ni kupata pointi 3 na sio idadi ya magoli," alisema Hamdi