Mshambuliaji wa Yanga Prince Dube jana aliibuka nyota wa mchezo wa ligi kuu dhidi ya KenGold uliopigwa uwanja wa KMC Complex, Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 6-1
Dube alipachika mabao mawili katika mchezo huo ambao alikuwa na nafasi ya kuondoka na hat-trik kama angetumia vyema nafasi
Lakini pia alitoa assist ya bao lililofungwa na Pacome Zouzoua na vilevile akahusika katika bao la 6 lililofungwa na Duke Abuya ambayo krosi yake iligeuzwa assist na Kennedy Musonda kwa Abuya

Dube amerejea rasmi katika mbio za ufungaji bora baada ya kufikisha mabao 7
Clement Mzize ndiye kinara wa mabao akifunga mabao tisa, nae alipachika mabao mawili jana. Dube na Pacome wote wana mabao 7
ADVERTISE HERE