Kesho Jumatano, Februari 05 katika uwanja wa KMC Complex, Yanga itakuwa na jambo lake itakapomenyana na KenGold katika mwendelezo wa ligi kuu ya NBC
Hii itakuwa siku maalumu kwa kiungo Khalid Aucho kwani itakuwa siku yake ya kupokea 'maokota' kutoka kwa mashabiki wa Yanga
Msimu huu mashabiki wa Yanga wamerasimisha ulee utaratibu wa kuwatuza wachezaji wanaofanya vizuri katika kila mechi katika dimba la KMC Complex
Clement Mzize, Pacome Zouzoua, Prince Dube, Mudathir Yahya na Maxi Nzengeli tayari wametembelewa na kibegi hicho cha 'maokoto' pale KMC Complex
Safari hii Wananchi wameona wampe heshima hiyo Aucho katika mchezo dhidi ya KenGold
Aucho amekuwa akifanya vizuri katika mechi nyingi lakini ni kama bahati mbaya kwake, ni nadra sana kupata tuzo
Sasa Jumatano ni siku nyingine ya kumtuza daktari huyo wa mpira...!