Nahodha Msaidizi wa Yanga Dickson Job amesema wachezaji wote wamejipanga kwa 'vita' ya kutetea ubingwa wao msimu huu
Baada ya mechi 16 za ligi kukamilika, Yanga imeendelea kusalia katika nafasi ya pili ikiwa na alama 42 nyuma ya watani zao Simba ambao wanaongoza msimamo wakiwa na alama 43
Lakini kwa mwenendo wa ushindani uliopo juu, yaonekana Yanga haina nafasi ya kufanya makosa katika mchezo wowote
"Ushindani ni mkali lakini sisi tumejipanga kupambana ili kuhakikisha tunatetea ubingwa wetu"
"Kila mechi kwetu ni kama fainali, tunapambana hadi mwisho," alisema Job
Jumatano, Februari 05 Yanga itashuka dimba la KMC Complex kuikabili KenGold ambapo baada ya mchezo huo, kituo kitakachofuata ni Mbweni dhidi ya JKT Tanzania, Februari 10
ADVERTISE HERE