Baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Kagera Sugar juzi, Jumatano Februari 05 Wananchi wanarudi tena uwanja wa KMC Complex kuikabili Ken Gold katika mwendelezo wa ligi kuu ya NBC
Mechi nyingine muhimu kwa Yanga kusaka ushindi ili kurudi tena kileleni mwa msimamo wa ligi
Ken Gold imesukwa upya ikisajili takribani wachezaji 23 katika usajili wa dirisha dogo
Miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa na timu hiyo ni Kelvin Yondani, Obrey Chirwa, Bernard Morrison na Erick Kabamba ambao wamewahi kuitumikia Yanga kwa nyakati tofauti
Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana katika mechi ya duru ya kwanza mkoani Mbeya, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0
Vijana wa kocha Sead Ramovic wamekuwa 'wa moto' wanapocheza dimba la KMC Complex wakigawa dozi 'nene' katika uwanja huo
Ken Gold watakuwa na kazi ya ziada kuzuia Gusa Achia Twenda Kwao ya Wananchi