Penalti zinavyomtesa Aziz Ki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Feb 2025
Penalti zinavyomtesa Aziz Ki

Jinamizi la kukosa mikwaju ya penati bado linamuandama kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki

Ndivyo unavyoweza kusema baada ya jana nyota huyo kukosa mkwaju mwingine katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar

Ni penati ya pili kukosa msimu huu kwenye ligi akiwa amefunga penati mbili tu katika penati 5 za mwisho alizopiga

Wanasema kukosa mkwaju wa penati kwa mchezaji ni sehemu ya mchezo lakini ni wazi takwimu zinaonyesha Aziz Ki anapaswa kuboresha umahiri wake katika kupiga 'matuta'

Hii ni changamoto ambayo inawakuta wachezaji wengi mahiri. Lionel Messi amewahi kukiri hadharani yeye sio mpiga penati mzuri, lakini huyu ndiye mchezaji bora zaidi aliyeshinda tuzo nyingi za Ballon d'Or

Licha ya kukosa mkwaju wa penati, Aziz Ki alikuwa na kiwango bora akitoa assist 1 katika ushindi wa mabao 4-0 ambao Yanga waliupata dhidi ya Kagera Sugar

Aziz Ki sasa amefikisha assist 5 msimu huu akiwa pia amefunga mabao mawili

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’