Ramovic apania ushindi dhidi ya Kagera Sugar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Jan 2025
Ramovic apania ushindi dhidi ya Kagera Sugar

Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic amesema wamejiandaa kwa mechi ngumu ya ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar ambayo itapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa KMC Complex

Akizungumza katika Mkutano na wanahabari mapema leo, Ramovic alisema Kagera Sugar ni timu ngumu na watahitaji kuwa bora katika mchezo huo ili kuibuka na ushindi

Ramovic alisema dhamira ya Yanga ni kushinda kila mchezo ili kurudi kileleni mwa msimamo wa ligi, hivyo watapambana ili kushinda mchezo huo

"Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu hivyo tunapaswa kucheza vizuri zaidi na kiukweli tunawaheshimu sana Kagera Sugar, Tunajua watakuja vizuri hasa kwa Kujilinda zaidi hivyo tunapaswa kutumia nafasi tutakazozitengeneza"

"Lengo letu kubwa ni kupata alama tatu kesho, sisi tunatazama zaidi mechi zetu na tuna jukumu la kushinda kila mchezo ili kurudi kileleni, tunajua ubora wa Kagera Sugar hivyo tuna jukumu la kucheza kwenye ubora wetu wa kila siku"

"Tuna mechi 15 mbele yetu, tunakwenda kucheza dhidi ya timu shindani kama tulivyo sisi, tunahitaji kushinda mechi zetu pasipo kuangalia matokeo ya wengine ili kuwa mabingwa," alisema Ramovic

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, beki Nickson Kibabage amesema wanatambua mechi dhidi ya Kagera Sugar itakuwa ngumu, wamejipanga kucheza kwa kumuheshimu mpinzani na muhimu kwao ni alama 3

"Kwa upande wetu sisi tumejiandaa vizuri na kila mchezaji anafahamu umuhimu wa Mchezo wa Kesho. Kikubwa ni kwamba tunawaheshimu sana Kagera Sugar kwasababu wana timu nzuri inayoleta Ushindani kwenye Ligi"

"Watakuja kuonesha ubora wao hivyo tunaamini utakuwa mchezo mzuri, Wananchi wategemee mazuri kutoka kwetu hapo Kesho," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
26m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’