Rais wa Yanga Injinia Hersi Said leo amekutana na kufanya mazungumzo na kiongozi wa Klabu ya AS Maniema Union ya DR Congo, Guy Kapya Kilongozi
Kwa mujibu wa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe, viongozi hao walikutana Morocco na kuzungumza masuala muhimu yanayozihusu klabu zao
Hata hivyo Kamwe hakuweka wazi masuala yaliyozungumzwa akidai ameelekezwa asiweke hadharani masuala hayo kwa sasa!
AS Maniema Union ndio klabu aliyotoka kiungo mshambuliaji wa Yanga Maxi Nzengeli lakini pia ndio klabu wanayocheza viungo Onoya Sangana (kiungo mkabaji) na Agee Basiala Amongo (kiungo mshambuliaji)
Kwa nyakati tofauti, Basiala na Onoya wametakiwa na klabu ya Yanga. Wananchi wasubiri taarifa ya Deal Done....?
ADVERTISE HERE