Ramovic amepania kuweka rekodi Ligi Kuu Bara

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Jan 2025
Ramovic amepania kuweka rekodi Ligi Kuu Bara

Kocha Mkuu wa Yanga, Sead Ramovic, ameweka wazi dhamira yake ni kuhakikisha Yanga inatetea mataji yake mawili yaliyobaki msimu huu na kujiwekea rekodi ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu akiwa kama kocha tangu atue barani Afrika

Kocha huyo ameyasema hayo siku chache kabla ya kuelekea kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa, Jumamosi kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam, dhidi ya Kagera Sugar

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ramovic, alisema baada ya kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kikosi chake kitakuwa na muda wa kujiandaa kwa ajili ya michezo ya ndani ambayo hataki kuacha kombe hata moja

Alisema Yanga ndiyo inayoshikilia makombe yote ya ndani, hivyo atahakikisha yanabaki, huku yeye mwenyewe akitaka kuweka rekodi ya kuyachukua kwa mara ya kwanza akiifundisha timu hiyo kongwe nchini

"Tunataka kushinda kila kitu, tunataka kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la FA, tumeshatolewa kwenye michuano ya kimataifa, nadhani sasa tuna muda mzuri wa kujiandaa"

"Inabidi sasa nguvu zetu zielekezwe huku, huu ndiyo mkakati ambao sasa tunao, na ili lifanikiwe tunatakiwa kushinda kila mchezo ulio mbele yetu, uwe wa Ligi Kuu au Kombe la FA, miguu ya wachezaji wetu inatakiwa kuwa na nguvu, ikimbie kilometa nyingi," alisema

Alisema yeye kama kocha kazi yake itakuwa moja tu kuwaelekeza wachezaji wake kwenye uwanja wa mazoezi nini cha kufanya watakapokuwa uwanjani, kwani na yeye anataka kuweka rekodi yake

"Kama kocha ni lazima unapokwenda sehemu na wewe uache alama," alisema kocha huyo ambaye alichukua nafasi ya Miguel Gamondi

Ramovic, ameiongoza Yanga kucheza michezo mitano ya Ligi Kuu, akishinda yote, ambapo Jumamosi wiki hii ataiongoza kwenye mechi ya sita

Alianza kuiongoza kwenye mchezo dhidi ya Namungo FC, uliopigwa Novemba 30, mwaka jana, Uwanja wa Ruangwa, Lindi, ikishinda mabao 2-0, Desemba 19, mwaka jana, kwenye Uwanja wa KMC Complex ikaizamisha Mashujaa FC 3-2, kisha ikaikanda Prisons 4-0, Desemba 22, mwaka jana, uwanja huo huo, kabla ya kwenda jijini Dodoma na kutoa kipigo kama hicho dhidi ya Dodoma Jiji na kumalizia kwa kutoa dozi ya mabao 5-0 dhidi ya Fountain Gate, Desemba 29, mwaka jana

Utakuwa ni mchezo wa mzunguko wa pili, ambapo wa kwanza ulichezwa Agosti 29, mwaka jana, Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera, Yanga ikipata ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Maxi Nzengeli na Clement Mzize

IPP Media

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14m ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’