Winga Mcongo aiomba Copco Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Jan 2025
Winga Mcongo aiomba Copco Fc

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Jonathan Ikangalombo ameisubiri kwa hamu mechi yake ya kwanza kuwatumikia mabingwa hao wa Tanzania Bara

Ikangalombo alitua Yanga katika dirisha dogo lililofungwa Januari 15, pengine kesho Jumamosi kocha Sead Ramovic anaweza kumtumia kwa mara ya kwanza katika mchezo wa raundi ya pili kombe la CRDB dhidi ya Copco Fc utakaopigwa dimba la KMC Complex

Winga huyo ambaye pia anamudu kucheza kama straika, amesema anatamani kuanza kuitumikia timu hiyo ili atoe mchango wake pia akieleza kuumizwa na matokeo ya mechi dhidi ya MC Alger ambayo yalisababisha Yanga isifuzu robo fainali ligi ya mabingwa

Nyota huyo aliyetua Yanga akitokea klabu ya AS Vita ya DR Congo,Β  hakutumika katika mechi dhidi ya MC Alger kwa vile alishaitumikia AS Vita katika mechi za awali za Kombe la Shirikisho Afrika na kibarua chake kipo katika mechi za mashindano ya ndani

"Nilikuwa naumia wakati nikiwa jukwaani kwani, niliona nina kitu ambacho kingeisaidia timu yangu, lakini kwa vile kanuni zilikuwa zinanizuia, sasa naomba nipewe mechi hizi za michuano ya ndani tuitafute tiketi ya CAF kwa msimu ujao," Ikangalombo alinukuliwa na Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’