Yanga kurejea Avic kujiandaa na FA, Ligi Kuu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Jan 2025
Yanga kurejea Avic kujiandaa na FA, Ligi Kuu

Baada ya mapumziko ya siku chache kikosi cha Yanga leo kinatarajiwa kurejea kambini Avic Town kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya kombe la FA dhidi ya Copco Fc itakayopigwa Jumamosi, na mechi za ligi kuu zinazorejea rasmi Februari 1

Imeelezwa Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic ametaka wachezaji wake wapate muda mrefu wa kukaa kambini akipinga utaratibu aliukuta ambao uliasisiwa na mtangulizi wake Miguel Gamondi ambapo timu ilikaa kambini angalau siku mbili kabla ya mechi

Baada ya kukabidhiwa mikoba ya kuinoa Yanga, Ramovic aliweka wazi kuwa wachezaji hawakuwa na fitness inayopaswa na hivyo kumpa wakati mgumu katika mechi za mwanzo

Hata hivyo katika miezi miwili Ramovic amefanya kazi kubwa ya kurejesha fitness ya wachezaji na kuinua viwango vyao na sasa anaamini wanapaswa kuendelea kuwa kambini kwa muda mwingi ili kuhakikisha wanalinda viwango na kujiimarisha zaidi

"Ni kweli timu ilikuwa inakaa kambini siku mbili hadi tatu kabla ya mchezo, kutokana na hilo kocha ameomba kuiona timu ikikaa kambini muda mrefu ili viwango vya wachezaji wake viendelee kuimarika bila kujihusisha na mambo mengine ambayo sio sahihi na kazi yao"

"Inaelezwa kuwa kocha havutiwi na viwango vya wachezaji kila wakitoka na kurudi majumbani kwao kwani siku wakikutana ni kama anaanza upya kuwaweka kwenye utimamu hali hiyo imemkwaza na kuwataka wachezaji warudi kutulia sehemu moja ili waweze kupambania taji la ligi na kombe la FA baada ya kushindwa kufikia malengo ya kucheza robo fainali," mtoa taarifa alibainisha katika mahojiano na Mwanaspoti

Ndani ya misimu mitatu mfululizo ambayo Yanga imekuwa na mafanikio makubwa, ilikuwa na utaratibu wa kuweka kambi Avic.

Kambi hiyo imefanikisha Yanga kuchukua mataji tisa yakiwemo matatu ya Ligi Kuu Bara, Kombe la FA (3) na Ngao za Jamii (3).

Chini ya makocha wawili walioipa mafanikio Yanga kwa misimu mitatu mfululizo wakianza na Nabi, Yanga ilitwaa mataji mawili ya ligi, Ngao ya Jamii (2) na Kombe la FA kisha kuifanya timu hiyo icheze fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2022-2023.

Chini ya Miguel Gamondi ambaye ameondolewa kikosini Novemba 2024, pia aliendeleza utamaduni wa Nabi kwa kuiweka timu kambini msimu mmoja wa mafanikio kwake akitwaa taji la ligi na Kombe la FA huku akicheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2023-2024 ikiwa ni rekodi baada ya kupita takribani miaka 25.

"Baada ya mafanikio hayo, utaratibu ulibadilika ambapo msimu huu wachezaji walikuwa wakiingia kambini siku chache kabla ya mechi na sio kukaa muda mrefu kama zamani"

"Hali hiyo taratibu ikaifanya timu kushuka kiwango na mwisho wa siku tukapoteza mechi mbili mfululizo za ligi hali iliyofanya Kocha Gamondi aondolewe na kuja Ramovic"

Tangu ajiunge na Yanga, Ramovic ameiongoza timu hiyo kucheza mechi 11 za kimashindano akishinda saba, sare mbili na kupoteza mbili

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
5h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’