Wakati Yanga ilipoweka hadharani kikosi kitakachoanza mchezo dhidi ya MC Alger jana, jina la kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua halikuwa katika orodha ya wachezaji walioanza mchezo huo
Ikumbukwe Pacome hakuonekana katika kikosi cha Yanga tangu timu iliporejea kutoka Mauritania ambako ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al Hilal
Jana baada ya mchezo kocha mkuu wa Yanga Sead Ramovic alithibitisha kuwa Pacome aliugua malaria siku chache kabla ya mchezo na hata kucheza kwake katika kipindi cha pili kulitokana na ujasiri wake
"Pacome ni mchezaji mzuri ambaye tunajivunia kuwa nae katika timu yetu. Wengi hawafahamu Pacome alikuwa mgonjwa, wiki yote amekuwa akisumbuliwa na malaria, hakuweza kufanya mazoezi kwa siku chache"
"Pamoja na mazingira hayo alijiona anaweza kuwa na mchango katika mchezo huu hasa katika kipindi cha pili"
"Amepambana kwa uwezo wake wote lakini mwishoni mwa tuliona nguvu yake ilikuwa inapungua," alisema Ramovic
Unaweza kusema Pacome ana bahati mbaya kwani mara nyingi zinapofika mechi muhimu za maamuzi anakuwa kwenye changamoto
Msimu uliopita alicheza mechi dhidi ya CR Belouizdad akiwa majeruhi huku akikosa mechi za robo fainali CAF CL dhidi ya Mamelodi Sundowns akiwa majeruhi