Mabadiliko Yanga hayaepukiki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 May 2018
Mabadiliko Yanga hayaepukiki
Msimu huu umetoa funzo kubwa kwa uongozi wa klabu ya Yanga kubadili mfumo wa uendeshaji wake haraka.

Kwa muda mrefu Yanga imekuwa ikitegemea zaidi fedha za wafadhili kuweza kutekeleza mahitaji yake.

Mafanikio iliyopata katika kipindi cha miaka 10 iliyopita yalitokana kwa kiasi kikubwa na uwekezaji uliokuwa ukifanywa na Yusuph Manji.

Kuondoka kwa Manji kumeiathiri Yanga kwa kiasi kikubwa na hakika ni moja ya sababu iliyopelekea kushindwa kutetea ubingwa wake msimu huu.

Ni wajibu wa kila Mwanachama kujitokeza kwenye Mkutano Mkuu mwezi ujao kuamua hatma ya Yanga.

Mpira wa sasa unahitaji uwekezaji mkubwa. Unahitaji wachezaji wazuri, makocha wazuri pia miundombinu mizuri.

Hivi huwezi kuvipata kama uwezo wa klabu kifedha ni mdogo.

Yanayotokea sasa Yanga ni matokeo tu ya 'bomu' tulilokuwa tukilipika kwa muda mrefu sasa linalipuka.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
6h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
11h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
11h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
15h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’