Beki Israel Mwenda anaweza kuitumikia Yanga katika michuano ya ligi ya mabingwa baada ya mchezaji huyo kuongezwa katika kikosi cha Wananchi kinachoshiriki michuano hiyo
Yanga imekamilisha usajili wa Mwenda kwa wakati kama ilivyokuwa kwa winga Jonathan Ikangalombo ambaye hata hivyo aliitumikia AS Vita katika mechi za awali kombe la Shirikisho la CAF msimu huu hivyo kukosa sifa ya kuitumikia Yanga katika michuano hiyo
Hata hivyo Ikangalombo ataweza kuitumikia Yanga katika mechi za ligi kuu na kombe la FA ambapo huenda akaanza kuonekana mwanzoni mwa Februari pale ligi itakaporejea
Tayari Bodi ya Ligi imetangaza mechi za viporo NBC PL zitapigwa wiki ya kwanza ya Februari ambapo Yanga itamenyana na Kagera Sugar mchezo utakaopigwa uwanja wa KMC Complex
Mwenda ametua wakati mwafaka katika kikosi cha Yanga kwani Yao Kouassi ni majeruhi na anaweza kuwa nje kwa takribani wiki sita
Mwenda ni mlinzi wa pembeni kiraka ambaye anaweza kutumika kama namba 2 au namba 3