Yanga imeenda Algeria, tuiombee

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 May 2018
Yanga imeenda Algeria, tuiombee
Kikosi cha Yanga kimeondoka jana jioni kuelekea nchini Algeria kikipita Dubai tayari kwa mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger unaopigwa keshokutwa May 06 nchini humo.

Yanga imeondoka huku wachezaji wake wakiwa na 'manun'guniko' ya madai ya hapa na pale.

Jana Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa alisema klabu hiyo inaendelea kutatua madai ya wachezaji wake kulingana na uwezo uliopo.

Mkwasa alisema CAF bado haijatoa zile Mil 600 na wanasubiri kupewa utaratibu wa namna watakazozipokea pesa hizo.

Baadhi ya wachezaji wameshindwa kujumuishwa katika safari hiyo ikielezwa wamegoma wakishinikiza uongozi uwalipe madai yao kwanza.

Wachezaji walioondoka jana jioni kwenda Algeria;

Youthe Rostand, Ramadhani Kabwili, Juma Abdul,Hassan Kessy, Haji Mwinyi, Gadiel Michael, Pato Ngonyani, Vicent Andrew, Abdallah Shaibu, Said Juma Makapu, Raphael Daudi, Pius Buswita, Yusuph Mhilu, Emmanuel Martin, Geofrey Mwashiuya, Juma Mahadhi na Yohana Mkomola.

Yanga inatarajiwa kuwasili nchini Algeria leo saa saba mchana
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
5h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
10h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’