Kikosi cha Yanga kilindoka Mauritania jana na timu kutua Addis Ababa, Ethiopia kwa ajili ya mapumziko
Leo Yanga inaunganisha ndege ya moja kwa moja kutoka Addis Ababa hadi jijini Dar es salaam ambapo kikosi kinatarajiwa kuondoka Ethiopia majira ya mchana
Yanga itakuwa na takribani siku tatu za kukamilisha maandalizi yake kuelekea mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya MC Alger
Mtanange huo wa kuipeleka Yanga robo fainali, utapigwa Jumamosi, Januari 18 katika uwanja wa Benjamin Mkapa




ADVERTISE HERE