Baada ya MC Alger kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya TP Mazembe jana wapo wanaoamini nafasi ya Yanga kufuzu robo fainali imekuwa finyu zaidi
Hata hivyo matokeo ya aina yoyote katika mchezo huo uliopigwa Algeria, yasingebadili malengo ya Yanga kushinda mechi zote mbili zilizobaki
Yanga haihitaji 'calculator' kujua hatma yake kwani, alama 6 za mechi mbili dhidi ya Al Hilal na MC Alger zitatosha kuwahakikishia Wananchi tiketi ya kutinga robo fainali
Zaidi hata kama Wananchi watapata sare dhidi ya Al Hilal, ushindi wa kuanzia mabao 2-0 dhidi ya MC Alger katika mchezo wa mwisho utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Januari 18, utatosha kuihakikishia Yanga kufuzu robo fainali
Hivyo malengo ya Yanga kuelekea mchezo dhidi ya Al Hilal hapo kesho ni kuhakikisha hawapotezi mchezo huo, ushindi ni kipaumbele lakini hata sare itaibakisha Yanga katika kinyan'ganyiro kuelekea mchezo wa mwisho nyumbani ambao utakuwa kama fainali
Msimu uliopita Yanga ilifuzu robo fainali nyumbani ikiwa na alama 8. Hata msimu huu Yanga inaweza kufuzu tena nyumbani ikiwa na alama 8 au 10!