Shungu amtabiria makubwa Ikangalombo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Jan 2025
Shungu amtabiria makubwa Ikangalombo

Wakati mabosi wa Yanga wakiwa mezani kumalizana na winga, Jonathan Ikangalombo, kocha wa zamani wa AS Vita anayotoka nyota huyo wa DR Congo, Raoul Shungu amefunguka juu ya makali ya mchezaji huyo akisema mabingwa wa Tanzania wamepata mtu wa kutengeneza mabao na kufunga.

Shungu aliyewahi kuzinoa Yanga na AS Vita kwa vipindi tofauti, alisema kama dili la nyota huyo litatiki Jangwani, basi timu yake hiyo ya zamani itakuwa imepata mtu wa maana mwenye uwezo wa kuisaidia kwani Jonathan ana pua ya kunusa nyavu na kusaidia wengine kutupia

Shungu alisema Jonathan ni winga asili wa kulia ambaye anajua kutengeneza nafasi za mabao akiwa na kasi na akili ya kuwapenya mabeki wa timu pinzani, mbali na kutengeneza nafasi pia ana uwezo wa kufunga, ambapo akiwa Vita alitengeneza safu bora ya ushambuliaji akisaidiana na Elie Mpanzu kabla naye hajatimkia Simba.

"Ikangalombo (Jonathan) ni winga mzuri anajua sana kutengeneza nafasi. Huyu anafaa kushambulia akitokea pembeni kulia au hata kushoto itategemea kocha wake atatakaje," alisema Shungu aliyewahi kuiongoza Yanga katika makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika 1998.

"Namjua Ikangalombo tangu akiwa Motema Pembe kabla ya kutua AS Vita, kwanza Yanga kama itampata imepata mchezaji mwenye adabu anayejua kutafuta maisha, sijawahi kuona akifanya mambo ya hovyo," alisema Shungu na kuongeza:

"Kitu kingine anajua pia kufunga, anajua kupunguza mabeki na kutengeneza nafasi mabeki wa timu pinzani watatakiwa kumchunga sana, akimudu pia kucheza kama mshambuliaji"

Katika msimu huu, rekodi zinaonyesha kuwa, Jonathan kwenye mechi 12 ambazo AS Vita inaongoza kundi la Ligi Kuu DR Congo, ametumika mechi sita, huku akikosa sita vilevile na amefunga bao moja na kuasisti mara mbili.

Shungu aliwatoa hofu mashabiki wa Yanga akisema licha ya winga huyo kutocheza mechi nyingi, lakini bado ana imani atakuwa na maisha mazuri ndani ya soka la Tanzania.

Shungu aliongeza, Yanga ya sasa haina winga asili kwenye kikosi chake na kwamba, Jonathan atakuwa mtu sahihi endapo kocha atahitaji kuwa na mtu mzuri atakayeshambulia kutokea pembeni.

"Hiyo kutocheza mechi sita sioni kama ni tatizo sana. Jambo zuri yupo sawa sasa kucheza, nadhani atafanya vizuri hapo Tanzania, ligi ya hapo naijua"

"Uzuri wake ni mtu mwenye nguvu anajua kupambana na mabeki. Bahati nzuri ni kwamba Yanga haina winga halisi, zaidi naona inawatumia viungo washambuliaji katika nafasi hizo. Huyu atawafaa sana kama watamalizana na kuanza kumtumia," alisema

Mchezo wa mwisho kwa Jonathan kuichezea AS Vita ulikuwa Novemba 24, mwaka jana katika dabi dhidi ya Renaissance akifunga bao pekee lililoipa ushindi timu hiyo akiibuka nyota wa mchezo

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’