Jana mashabiki na baadhi ya mastaa wa Yanga walifanya manunuzi katika duka la nguo na vifaa vya michezo linalomilikiwa na mshambuliaji Celemnt Mzize lililoko Sinza jijini Dar es salaam
Baada ya kuwapa furaha Wananchi katika mchezo dhidi ya TP Mazembe juzi, akifunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-1 uliofufua matumaini ya Yanga kufuzu robo fainali, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe aliwaongoza Wananchi na wanahabari katika tukio hilo la aina yake la kutembelea duka la Mzize na kufanya manunuzi
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said na Makamu wa Rais Arafat Haji ni miongoni mwa waliomchangia Mzize katika kuimarisha biashara yake wakichangia Tsh Milioni 2.5
Nahodha msaidizi wa Yanga Dickson Job na kiungo mshambuliaji Stephan Aziz Ki ni miongoni mwa waliofika dukani kwa Mzize wakiungana na mamia ya Wananchi waliofanya manunuzi jana






