Robo fainali inawezekana - Ramovic

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Jan 2025
Robo fainali inawezekana - Ramovic

Kocha mkuu wa Yanga, Sead Ramovic amesema hadi sasa hesabu za timu hiyo katika Ligi ya Mabingwa Afrika zipo sawa baada ya kuifumua TP Mazembe kwa mabao 3-1 na kudai kipigo hicho ni kidogo kuliko nafasi walizotengeneza, huku mshambuliaji Clement Mzize akiwashtua Wakongo Kwa Mkapa.

Yanga ilipata ushindi huo katika mechi ya raundi ya nne ya Kundi A na kumfanya Ramovic aamini, wana hesabu sahihi za kutinga robo fainali japo wamesaliwa na vikwazo viwili mbele yao dgidi ya Al Hilal na MC Alger

Ramovic amewapongeza wachezaji wake kwa kushika haraka na vizuri falsafa alizowapa akiwa na imani kuwa wanaweza kushinda mbele ya Al Hilal wikiendi hii ugenini, kisha kurudi nyumbani kuikaribisha MC Alger Januari 18

"Ni matokeo yaliyotupa imani kuwa, bado tunaweza kufanya kitu kufikia lengo la kutinga robo fainali, hii ni mechi kubwa tumeiamua kwa nguvu kubwa ya ubora wetu," alisema Ramovic na kuongeza

"Tunahitaji kuendeleza matokeo kama haya katika mechi mbili zinazofuata, nafurahi namna wachezaji wanavyoendelea kuimarika, tunacheza mpira tunaotaka tuucheze kwa kumnyima mpinzani nafasi ya kupumua"

Ramovic pia alisema juzi, Yanga ilistahili kushinda kwa idadi kubwa ya mabao zaidi, kwani ilitengeneza nafasi nyingi hasa kipindi cha kwanza na hata cha pili ilipofunga mawili muhimu baada ya kwenda mapumziko wakiwa nguvu sawa ya 1-1 na Mazembe.

"Tunawaheshimu sana wapinzani wetu (Mazembe) lakini tulistahili ushindi mkubwa zaidi jana (juzi) tungeweza kufunga mabao matano hadi sita kama tungeongeza umakini. Ilikuwa ni mechi yenye presha kubwa ya ushindi kwa kila mchezaji lakini tuliendelea kuwatuliza wacheze kwa umakini ili tupate tunachokitaka"

Akimzungumzia mshambuliaji Clement Mzize aliyepachika mabao mawili katika mchezo huo, Ramovic alisema bado anahitaji mwaka mmoja kumzungumzia anafiti nafasi ipi uwanjani.

Kocha huyo alisema hana winga asilia, kiungo mshambuliaji asilia wala beki namba mbili asilia ndio maana amekuwa akifanya mabadiliko kila mara kusaka mchezaji anayefiti nafasi hizo akimgusia zaidi Mzize ambaye ni mshambuliaji anayemtumia zaidi pembeni kama winga na amekuwa akimpa matokeo mazuri.

"Siwezi kusema Mzize sasa nitamtumia kama winga kwa vile amefanya vizuri juzi akifunga mara mbili, hapana nimekuwa nikifanya mabadiliko kila mara nikiwa natafuta nafasi sahihi kwa kila mchezaji akiwamo yeye (Mzize)," alisema Ramovic na kuongeza;

"Ndio maana kiungo mshambuliaji naweza nikamtumia kama mshambuliaji wa mwisho na straika akatumika kama winga, hivyo kuhusu nafasi sahihi ya Mzize naomba niulizwe tena baada ya mwaka mmoja," alisema Ramovic

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’