Mwamuzi Daniel Nii Ayi Laryea wa Ghana ndiye atachezesha mechi ya ufunguzi ya hatua ya 16 Bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya wenyeji, U.S.M Alger dhidi ya Yanga SC ya Tanzania Jumapili May 06 mjini Algiers, Algeria.
Pamoja na Laryea, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limewateua Abel Baba wa Nigeria na David Laryea wa Ghana pia kuwa waamuzi wasaidizi, maarufu kama washika vibendera katika mchezo huo wa Kundi D uliopangwa kuanza Saa 2:00 usiku na Saa 4:00 usiku kwa saa za Tanzania.
Yanga Sc inatarajiwa kuondoka nchini kesho kwenda Algiers kwa ndege ya Emirates Air ikipitia Dubai tayari kwa mchezo huo wa kwanza wa Kundi D Kombe la Shirikisho la Soka Afrika.
Pamoja na Yanga na USM Alger, timu nyingine katika Kundi D ni Rayon Sport ya Rwanda na Gor Mahia ya Kenya ambazo zitamenyana zenyewe katika mchezo wa ufunguzi wa hatua ya 16 Bora ya Kombe Shirikisho Afrika.
Bin Zubeiry

ADVERTISE HERE