Wachezaji Kennedy Musonda, Maxi Nzengeli na Aziz Andabwile jana walishiriki mazoezi ya kikosi cha Yanga kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Fountain Gate utakaopigwa kesho Jumapili katika uwanja wa KMC Compex
Musonda alishiriki mazoezi na wachezaji wengine hiyo ikiwa ni ishara kuwa yuko tayari kutumika katika mchezo unaofuata huku Nzengeli na Andabwile wakianza na mazoezi mepesi

Wachezaji ambao bado wako nje ni mlinda lango Djigui Diarra na kiungo Clatous Chama
Diarra anaendelea na matibabu ya misuli wakati Chama anauguza jeraha la kiwiko wote wakiumia katika mchezo dhidi ya TP Mazembe
Kurejea kwa nyota hao ni habari njema kwa Yanga ambayo inawahitaji katika mapambano yake ya kutetea ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa nne mfululizo na kufuzu robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika