Kikosi cha Yanga kesho Alhamisi kitasafiri kuelekea Algeria tayari kwa mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya kombe la shirikisho dhidi ya wenyeji USM Algers.
Mchezo huo utapigwa Jumapili ijayo, May 06 nchini Algeria.
Meneja wa Yanga Hafidh Saleh ameuambia mtandao rasmi wa klabu hiyo kuwa matayarisho ya mchezo huo yanakwenda vizuri na ni kiu ya kila mmoja kikosini kuona timu inaibuka na matokeo mazuri ili kutengeneza mazingira salama kwenye kundi.
"Tuko sawa tumejiandaa, tunahitaji kupata matokeo mazuri, ili kujenga ari mpya katika adhma yetu ya kufanya vizuri kimataifa,hatua ya makaundi ni ngumu kwa sababu kila mchezo unakutana na timu ngumu,nia yetu msimu huu tufike mbali zaidi kuliko miaka yote iliyopita," amesema.
Baada ya kuwavaa USM Alger, mchezo wa pili utapigwa May 16 dhidi ya Rayon Sport.

ADVERTISE HERE