Beki kiraka wa Yanga Kibwana Shomari amewashukuru mashabiki kwa sapoti yao kwake katika nyakati zote alizopitia
Baada ya kutoonekana uwanjani kwa muda mrefu, jana kocha Sead Ramovic alimuanzisha Kibwana katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mashujaa Fc, Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 3-2 katika uwanja wa KMC Complex
Pengine ndio mechi ambayo inaweza kumrejesha tena Kibwana katika kikosi cha kwanza kwani alionyesha kiwango kikubwa akihusika katika upatikanaji wa bao la kwanza na baadae kutengeneza bao l tatu
Kibwana amesema mashabiki wa Yanga walimtia moyo katika nyakati ngumu na wameendelea kumuunga mkono hata sasa
Wakati mchezo ukiendelea kila Kibwana alipogusa mpira majukwani zilisikika kelele za mashabiki wakiimba jina lake
"Nawashukuru sana mashabiki wa Yanga, wakati nilipokuwa sichezi walinitia moyo niendelee kupambana, leo kocha ameniamini, amenipa nafasi na nimeisaidia timu yangu kupata ushindi"
"Kikubwa nilifuata maelekezo ya mwalimu kabla ya mechi aliniambia hujacheza muda mrefu leo nakupata nafasi, ukafanye vyema uisaidie timu"
"Nashukuru nimetoa assist moja ya bao la tatu na pressing niliyofanya pia ilisaidia kupatikana bao la kwanza," alisema Kibwana
Kibwana alitumika kwa dakika 71 katika mchezo huo, Wananchi wamefurahishwa na kile alichofanya