Yanga Princess leo imeshindwa kutamba mbele ya JKT Queens ikikubali kipigo cha mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa KMC Complex
Ni kipigo cha pili kwa Yanga Princess msimu huu wa ligi kuu ya Wanawake ikiwa pia imepoteza mchezo dhidi ya watani zao Simba Queens na kutoka sare mechi nyingine tatu pia wakishinda mechi mbili tu
Itoshe kusema huu ni msimu mwingine wa kuijenga Yanga Princess imara, Kocha Edna Lema bado ana kazi ya kufanya katika uwanja wa mazoezi
Yanga Princess bado inahitaji kuimarishwa zaidi kwani daraja lao la ushindani liko chini kulinganisha na JKT Queens na Simba Queens
ADVERTISE HERE