Tukemee matukio ya vurugu viwanjani - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Dec 2024
Tukemee matukio ya vurugu viwanjani - Kamwe

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema matukio ya vurugu viwanjani yanapaswa kulaaniwa vikali kwani yanachafua taswira ya nchi

Kamwe ametoa kauli hiyo baada ya kile kilichotokea uwanja wa Benjamin Mkapa jana kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho kati ya Simba dhidi ya CS Sfaxien ambapo mashabiki wa Simba walin'goa viti kuwashambulia mashabiki wachache wa CS Sfaxien baada ya vurugu kuibuka mchezo ulipomalizika

Serikali imeagiza klabu ya Simba ilipe gharama za uharibifu huo ambapo viti 256 vilin'golewa majukwaani

Kamwe amewataka wanahabari kukemea tukio hilo kwani madhara yake katika soka la Tanzania ni makubwa

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Kamwe ameandika ujumbe huu;

Ndugu zangu Wanahabari, kama kuna Kosa kubwa Tunalifanya ni kutumia ‘kivuli cha uzalendo’ kutetea vitendo vya Kipuuzi vilivyofanyika Jana uwanja wa Mkapa

Madhara ya Lile Tukio ambalo tayari Liko kwenye mjalada Afrika hivi sasa ni Makubwa mno kwenye Mpira wetu na Taifa Letu kwa ujumla kuliko Faida ya Pointi 3 zinazoshangiliwa

Mpira hauchezwi kwetu peke yake, Ziko nyakati tutatakiwa kusafiri kwenda ugenini kucheza

Na itakayosafiri sio Timu moja tu, timu nyingi zinasafiri, za mpira wa miguu mpaka Mchezo wa Draft, Na ni kuanzia Levo ya Klabu hadi Timu za Taifa.

Vipi kama Leo tukiona ni sawa kuliweka jina la Tanzania kwenye Uhuni huu? Nini yatakuwa matokeo yake pindi Watanzania wenzetu wakienda kwenye hizo nchi tunazozipiga?

Leo Tunacheka na kufurahi, Lakini tumewaza Watunisia wanapanga kufanya nini kwao? Usalama wa Watanzania wenzetu watakaosafiri utakuwa vipi? Waandishi wa Habari ambao mara nyingi mnakaa eneo la Media bila ulinzi, Usalama wenu utakuwa vipi?

Basi tunaweza tusisafiri, Mashabiki na Waandishi kwa sababu ya hofu, vipi Watanzania wanaoishi Tunisia? Tumewafikiria maisha yao watakapokanyaga uwanjani?

Tafadhali sana, Tusitetee huu Upuuzi na Uhuni wa Jana pale uwanja wa Mkapa kwa ‘mwamvuli wa Uzalendo’. Jambo hili Tayari Liko wazi na Limeshaweka DOA MPIRA WETU

Ni vyema Tukemee jambo hili, Na kama tukishindwa kwa sababu ‘huwa Tunalipwa kusifia’ basi Busara ni Tukae kimya bila kuwanyamazisha au kuwazodoa wanaokemea.

Wanaokemea wanakemea UHUNI VIWANJANI. Wanakemea kulinda Taswira ya Mpira na Taifa Letu kwa Ujumla.

Na kama Kweli mmejaa Uzalendo mnaosema, tungewaona ni watu wa maana kweli kama mngeanza kukemea au Kutoa Pole kwa Watanzania wenzenu waliopigwa DR Congo

Yaliowakuta Yanga Congo mlifunga vinywa vyenu, Yamewatoa Maboss zenu mmekuwa mstari wa mbele kutetea na kupiga vita wanaozungumza. Hii sio sawa.

Naiomba Serikali na Shirikisho la Mpira wa Miguu, TFF kuchukua Hatua za haraka Kupambana na Wahuni wote waliofanya uhuni huu siku ya jana na Itangazwe wazi bila kuficha ficha kwa Faida kubwa ya Mpira wetu na Taifa letu kimichezo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’