Jana Al Hilal waliichapa MC Alger bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa July 05 1962 nchini Algeria
Ushindi huo unaiweka Al Hilal katika nafasi nzuri ya kutinga robo fainali kwani kimahesabu wanahitaji alama 1 tu kutoka mechi tatu zilizobaki ili wafuzu
Lakini pia matokeo ya mchezo huo, yanafanya kundi A kuwa wazi zaidi kwani Mc Alger, Yanga na TP Mazembe sasa zina nafasi sawa ya kufuzu, itakuwa vita ya kuwania nafasi ya pili
Habari njema kwa Yanga ni kuwa mechi mbili kati ya tatu zilizobaki zitapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa wakati MC Alger na TP Mazembe kila moja imebaki na mechi moja tu nyumbani
Kama Yanga itashinda mechi zake mbili nyumbani itakuwa na uhakika wa kufikisha alama 7 na muhimu Yanga inapaswa kuhakikisha haipotezi mechi dhidi ya Al Hilal ugenini ili kuwa katika nafasi nzuri
Mechi tatu zilizobaki zitakuwa kama fainali kwa Yanga