Bao alilofunga Prince Dube leo katika mchezo dhidi ya TP Mazembe lina thamani kubwa kwa klabu ya Yanga na hata kwake mwenyewe
Baada ya kupita kipindi kirefu cha kutofunga, akivumilia kashfa na dharau kutoka kwa wasiomtakia mema, Dube leo amefunga bao ambalo litawakumbusha wale walioanza kusahau umahiri wake
Alikuwa eneo sahihi kwa wakati sahihi akauwahi mpira uliotemwa na mlinda lango wa TP Mazembe
Pengine ni bao ambalo litamrudishia kujiamini kwake na kuendelea kufunga katika mechi zinazofuata
Kwa Yanga ni alama 1 moja muhimu ambayo kimahesabu inaweza kuwa sababu ya Yanga kufuzu robo fainali
Hesabu za Yanga sasa ni kushinda mechi mbili zilizobaki nyumbani na kuhakikisha haipotezi ugenini mechi ya mwisho dhidi ya Al Hilal
Kimahesabu Yanga inaweza kufikisha alama 10 ambazo zitatosha kwenda robo fainali