Tutarekebisha makosa yetu - Nsajigwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 May 2018
Tutarekebisha makosa yetu - Nsajigwa
Mabingwa watetezi ligi kuu ya Vodacom Yanga juzi walikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa mahasimu wao Simba hivyo kuuweka reheni ubingwa wao ambao bila shaka unaelekea kwa watani zao Simba.

Kocha msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema kipigo walichokipata juzi kimetokana na makosa yaliyokuwa yakifanywa na wachezaji wake hasa eneo la kiungo.

"Tulifanya makosa mengi, Simba walitumia mapungufu yetu kupata lile bao, hatukuwa vizuri kwenye eneo la kiungo, lakini pia safu ya ulinzi hatukuwa imara kwenye mipira ya krosi," alisema Nsajigwa.

Aidha, alisema mabadiliko aliyoyafanya ya kumtoa Papy Tshishimbi na Ibrahim Ajibu ambayo yalilalamikiwa na mashabiki wengi, yalikuwa ya kiufundi zaidi.

"Tshishimbi hakuwa kwenye ubora wake na hata Ajibu, tulifanya mabadiliko ya kuwatoa na kuwaingiza Mahadhi (Juma) na Buswita (Pius) ili kuongeza nguvu ya ushambuliaji," alisema Nsajigwa.

Alisema kwa kusaidiana na kocha mpya wa timu hiyo ambaye juzi hakuwa kwenye benchi kutokana na kutokamilika kwa vibali vya kufanyia kazi, Mkongoman Mwinyi Zahera, watafanyia kazi haraka mapungufu waliyoyaona.

"Tuna michezo ya Kombe la Shirikisho Afrika, tutahakikisha tunafanyia kazi kile tulichokiona ili kujiandaa vyema na mechi hizo na michezo mingine iliyobakia ya Ligi Kuu," alisema Nsajigwa.

Yanga itacheza mchezo wake wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger ya Algeria mwishoni mwa wiki hii.

Inatarajiwa kuondoka keshokutwa May 03 kwenda nchini Algeria
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’