Yanga Princess leo imeandikisha ushindi wa pili mfululizo katika ligi kuu ya Wanawake (WPL) ikipata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Mlandizi Queens
Mabao ya Yanga Princess yalipachikwa na Neema Paul aliyefunga mabao mawili, Aisha Omary na Neema Shau wakifunga bao moja kila mmoja
Yanga Princess sasa imekusanya alama 9 katika mechi 6 ikisogea hadi nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi
Simba Queens wanaongoza ligi hiyo wakiwa na alama 15 huku JKT Queens wakishika nafasi ya pili wakiwa na alama 13
JKT Queens itachuana na Simba Queens katika mchezo mwingine wa ligi hiyo utakaopigwa kesho
ADVERTISE HERE