Kikosi cha Yanga kilitua Dubai jana usiku wakitoka Algeria baada ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya MC Alger uliopigwa juzi
Leo Yanga inaunganisha ndege nyingine kutoka Dubai kurejea jijini Dar es salaam ambapo kikosi kinatarajiwa kuwasili JNIA saa 7 mchana
Yanga itakuwa na siku chache za kukamilisha maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi ya TP Mazembe utakaopigwa Jumamosi huko DR Congo
Hii ni mechi ambayo Yanga haipaswi kupoteza ili kuweka hai matumaini ya kusonga mbele
Jana TP Mazembe walikubaki kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Al Hilal na kuwafanya wasalie na alama moja katika nafasi ya tatu kundi A
Mechi zote mbili zinazofuata ambazo Yanga inakipiga na TP Mazembe zitakuwa kama fainali
ADVERTISE HERE