Baada ya kupoteza mchezo wa pili wa ligi ya mabingwa dhidi ya MC Alger hapo jana, kikosi cha Yanga leo asubuhi kimefanya mazoezi ya 'recovery' kabla ya kuanza safari ya kurejea Dar wakipitia Dubai
Yanga inalazimika kurudi Dar mapema kukamilisha maandalizi yake kabla ya kuelekea DR Congo kuikabili TP Mazembe, Jumamosi ijayo, Disemba 14
Katika mechi nne zilizobaki kwenye michuano ya ligi ya mabingwa, mechi mbili zitapigwa ugenini na nyingine mbili ni nyumbani
Mechi ya marudiano dhidi ya TP Mazembe itapigwa Januari 03 2025 na baadae Yanga kusafiri Mauritani kuikabili Al Hilal Januari 10 2025
Yanga itamaliza kampeni yake ya kuwania tiketi ya kutinga robo fainali ikiwa nyumbani kwa mchezo wa marudiano dhidi ya MC Alger ambao utapigwa Januari 17 2025
Kuna msemo maarufu 'HAIJAISHA MPAKA IISHE', hivi ndivyo Yanga inakwenda kuzikabili mechi nne zilizobaki