Yanga ipo tayari kuwapa furaha Wananchi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Dec 2024
Yanga ipo tayari kuwapa furaha Wananchi

Mlinda lango Djigui Diarra leo huenda akarejea langoni katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa dhidi ya MC Alger

Diarra aliyekosa mechi iliyopita dhidi ya Namungo Fc kutokana na majeraha, alishiriki kikamilifu mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo huo utakaopigwa saa 4 usiku

Nyota wengine waliokuwa majeruhi Chadrack Boka na Clement Mzize nao jana walishiriki mazoezi ya mwisho lakini kuna nafasi ndogo kwao kutumika katika mchezo wa leo

Nahodha Msaidizi Dickson Job nae yuko 'fit' licha ya kufanya mazoezi akiwa amefunga 'bandeji' kwenye goti lake la kulia kutokana na majeraha aliyopata katika mchezo uliopita dhidi ya Namungo Fc

Hata hivyo daktari wa Yanga Moses Etutu amesema majeraha hayo yalikuwa ya kawaida na hayatamzuia kucheza leo kama kocha Sead Ramovic ataamua kumtumia

Kiungo Khalid Aucho naye yuko 'fit' bila atakuwa tayari kushuka dimbani leo kama Ramovic atamuhitaji katika kikosi chake leo

Baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika mchezo uliopita dhidi ya Namungo Fc, nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto huenda akapata nafasi ya kuanza katika safu ya ulinzi leo huku Kennedy Musonda aliyefunga bao katika mchezo dhidi ya Namungo Fc akitarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji

Kiungo Clatous Chama pia leo anaweza kuanza baada ya kuwa na takribani dakika 40 bora katika mchezo dhidi ya Namungo Fc

Ramovic leo anatarajiwa kutumia kikosi chake imara ambacho kitampa uwiano mzuri katika kushambulia na kujilinda kwa kuwa ni mechi ya ugenini

Yanga inahitaji ushindi au hata matokeo ya sare leo ili kutovuruga malengo ya kuvuka hatua ya makundi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’