Kupoteza mchezo dhidi ya mpinzani wako wa jadi ni matokeo ambayo hakuna mshabiki anayependa kuyasikia lakini misho wa siku yabidi kukubali.
Baada ya matokeo haya Yanga inabidi kujipanga zaidi kwa ajili ya kumaliza michezo iliyobaki kukamilisha msimu lakini sasa ielekeze nguvu kwenye michuano ya kombe la Shirikisho CAF CC ambayo Jumapili ijayo itakuwa ugenini nchini Algeria kuumana na USM Alger.
Kipigo cha leo ni dhahiri kimeiondolea Yanga matumaini ya kutetea ubingwa wake kwa msimu wa nne.
Mchezo wa leo haukuwa mzuri sana kwa upande wa Yanga, mzungu wa simba alifanikiwa kwa kiasi kikubwa na mbinu zake.
Nadiriki kusema timu bora imeshinda siku ya leo.
Sio jambo jema kuwatupia lawama wachezaji na benchi la ufundi kwani wao wamejitahidi kadiri ya uwezo wao.
Walinzi Kelvin Yondani na Andrew Vicent Chikupe wanastahili pongezi sana kwa uhodari wao siku ya leo.
Walifanikiwa kuwadhibiti Bocco na Okwi na hata bao walilopata Simba lilitokana na makosa ambayo hawawezi kulaumiwa
Sote tunatambua misukosuko iliyopitia Yanga msimu huu, hapa ilipofika ni mafanikio makubwa kwao.
Wachezaji wa Yanga wanapaswa kupongezwa kwa upambanaji wao licha ya mazingira waliyopitia lakini pia inafaa kuwapa moyo ili wafanye vizuri kwenye michuano ya CAF CC

ADVERTISE HERE