Baada ya kutua Algiers jana, kikosi cha Yanga kililazimika kusubiri uwanja wa ndege kwa takribani saa nne kukamilisha taratibu kabla ya kuruhusiwa kwenda Hotelini
Yanga iliondoka Dubai mapema asubuhi na kutumia takribani saa 7 na nusu angani kabla ya kutua Algiers ambako pia walikaa saa 4 uwanja wa ndege na kufanya timu kutumia zaidi ya saa 11 mpaka kuingia Legacy Luxury Hotel walipofikia
Habari njema ni kuwa mchezo utapigwa siku ya Jumamosi, wachezaji wamepata muda wa kutosha wa mapumziko ambapo leo kikosi kitafanya mazoezi ya kwanza hapo Algeria
Yanga inahitaji kushinda mchezo dhidi ya MC Alger au hata sare ili kuweka hai malengo ya kufuzu robo fainali
Vijana wa kocha Sead Ramovic wanahitaji 'kufidia' matokeo ya kupoteza mechi ya kwanza nyumbani ili kuwa katika nafasi nzuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu