Ushindi dhidi ya Namungo umeongeza mzuka Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Dec 2024
Ushindi dhidi ya Namungo umeongeza mzuka Yanga

Wachezaji wa Yanga wamekiri kuwa walikuwa kwenye wakati mgumu baada ya kupoteza michezo mitatu mfululizo, kitu ambacho si cha kawaida kwa timu kubwa kama hiyo

Lakini ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo Fc juzi ni kama umepunguza presha iliyokuwa ikiwakabili na kuwaongezea mzuka kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya MC Alger utakaopigwa Jumamosi huko Algeria

"Mchezo dhidi ya Namungo haukuwa rahisi kama watu walivyodhani, ulikuwa mgumu kwa sababu kuna presha ambayo ilianza kuingia kwenye timu baada ya kupoteza mechi zetu mbili za Ligi Kuu na ile ya kimataifa dhidi ya Al Hilal"

"Kikubwa kupoteza michezo ile maana yake tulikuwa nje ya malengo, lakini wachezaji tulitulia na kuangalia nini kinahitajika ili turejeshe makali yetu, kweli tumefanya hivyo na tumeshinda dhidi ya Namungo, ushindi ambao umetuweka vizuri sasa kuelekea kwenye mchezo wetu wa Jumamosi," alisema nahodha msaidizi wa Yanga Dickson Job

Nae nyota wa mchezo huo, Duke Abuya, alisema ushindi walioupata unakwenda kwa mashabiki na kuwaomba msamaha baada ya kuwapa huzuni na kuwavunja nguvu, akiahidi kuwa hilo halitatokea tena la kupoteza michezo mitatu mfululizo

"Tulikuwa kwenye wakati mgumu sana, kupata huu ushindi kimekuwa kitu cha maana sana, kimeturudisha wachezaji kwenye msitari"

"Nawaomba wachezaji wenzangu tuendelee na mwendelezo huu, tumewavunja nguvu na kuwahuzunisha mashabiki wetu, lakini sasa tuwafanye warudishe furaha yao walioizoea, niwaambie kuwa waendelee kutusapoti na hatutowaangusha tena," alisema Abuya

Yanga inaondoka leo kuelekea Algeria tayari kwa mchezo dhidi ya MC Alger, Wananchi wakihitaji kushinda mchezo huo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’