Yanga kumburuza kortini Ahmed Ali

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Dec 2024
Yanga kumburuza kortini Ahmed Ali

Klabu ya Yanga imemtaka Meneja habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally kutoka hadharani na kuomba radhi kwa matamshi ya kuichafua klabu ya Yanga

Aidha Yanga imemtaka Ahmed kulipa fidia ya Tsh Bilioni 10 kutokana na kauli aliyotoa hivi karibuni

Katika moja ya mahojiano aliyofanya, Ahmed alisikika akitoa kauli hii;

Β "Pacome amemaliza mkataba tukiona anafaa tutahangaika nae, Pacome amemaliza mkataba ndani ya Yanga na hana mpango wa kuongeza"

"Mtanyoa ndevu mwaka huu hana mpango wa kuongeza amechoka kuchomwa sindano kila siku kama anazuia mimba"

"Tunaangalia kiwango chake kama kitaturidhisha tutahangaika nae lakini kama ataendelea na mwenendo wake anaoendelea nao tutawaachia kama tulivyowaachia Chama na tunataja majina Live hakuna kutumia code"Β 

Taarifa ya madai ya Yanga imeeleza kuwa kauli hiyo ni ya upotoshaji na imejaa dharau kwa klabu yao, hivyo imeharibu mahusiano yao na wadau wa kibiashara na wadhamini

Yanga wamemtaka Ahmed afanye yafuatayo ndani ya siku tano (5);

  1. Kuomba radhi kwa njia sawa na aliyotumia kutoa kauli yake
  2. Kufidia malipo ya Tsh Bilioni 10 (10,000,000,000)

Yanga imetahadharisha kuwa kama maagizo hayatafanyiwa kazi watafuata hatua za kisheria zaidi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Aziz Ki ameanza kwa kusuasua lakini namba zinaongea
Aziz Ki ameanza kwa kusuasua lakini namba zinaongea
30m ago
READ MORE β†’
Nini matarajio Fadlu kutua Yanga?
Nini matarajio Fadlu kutua Yanga?
2h ago
READ MORE β†’
Maxi na msimu wa maajabu Yanga
Maxi na msimu wa maajabu Yanga
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 06 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 06 2026
6h ago
READ MORE β†’
Abuya, Yao warejea mazoezini baada ya kupona majeraha
Abuya, Yao warejea mazoezini baada ya kupona majeraha
16h ago
READ MORE β†’
Mpango wa kumshusha Ramovic umekwama, Yanga yarudi kwa Fadlu
Mpango wa kumshusha Ramovic umekwama, Yanga yarudi kwa Fadlu
21h ago
READ MORE β†’
Dladla amejihakikishia nafasi yake Yanga
Dladla amejihakikishia nafasi yake Yanga
1d ago
READ MORE β†’
Happy Birthday Mwamnyeto
Happy Birthday Mwamnyeto
1d ago
READ MORE β†’
Novemba 5 itaendelea kukumbukwa na Wananchi
Novemba 5 itaendelea kukumbukwa na Wananchi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi Novemba 05 2026
Magazeti ya leo Alhamisi Novemba 05 2026
1d ago
READ MORE β†’