Baada ya ushindi dhidi ya Namungo Fc juzi, kikosi cha Yanga kinarejesha makali yake katika michuano ya ligi ya mabingwa ambapo Jumamosi Disemba 07 kitakuwa ugenini Algeria kuchuana na MC Alger katika mchezo wa pili kundi A
Hii ni mechi muhimu kwa Yanga kuhakikisha haipotezi ili kuweka hai matumaini ya kutinga robo fainali
Baada ya mchezo huo Yanga itasafiri Lubumbashi DR Congo kuwakabili TP Mazembe katika mchezo wa raundi ya tatu CAF CL dhidi ya TP Mazembe ambao utapigwa Disemba 14
Wakitoka DR Congo Wananchi watarejea Dar kucheza mechi mbili za ligi kuu dhidi ya Mashujaa Fc (Dec 19) na Tanzania Prisons (Dec 22)
Disemba 25 Yanga itakuwa Dodoma kuchuana na Dodoma Jiji kisha kurejea Dar kufunga mwaka 2024 kwa mchezo dhidi ya Kagera Sugar Disemba 29