Mwamnyeto ni kiongozi wa mfano uwanjani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Dec 2024
Mwamnyeto ni kiongozi wa mfano uwanjani

Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic amempongeza nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto kwa kiwang bora alichoonyesha katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc jana

Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Majaliwa, Ruangwa Mwamnyeto akirejea kikosini akichukua nafasi Ibrahim Bacca anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu

Ramovic alisema Mwamnyeto ni mchezaji wa mfano kwa wenzake,anajituma, ni kiongozi bora katika kikosi chake

"Kipekee nampongeza nahodha wetu, Mwamnyeto amekuwa na mchezo mzuri. Ni mchezaji wa mfano iwe katika mechi hata tunapokuwa mazoezini,"alisema Ramovic

Mwamnyeto anaonekana kurejea katika ubora wake baada ya kupitia kipindi kifupi cha changamoto ambacho kilipelekea kupoteza nafasi yake katika kikosi cha kwanza

Wakati mwingine ni bahati mbaya kwake kwani pale anapofanya vizuri huwa hazungumziwi lakini wakosoaji wake wanasubiri pale anapofanya makosa

Jana aliiongoza vyema safu ya ulinzi akizuia na kuanzisha mashambulizi pale alipohitajika

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ratiba ya mwisho wa mwaka usipime
Ratiba ya mwisho wa mwaka usipime
2h ago
READ MORE β†’
Adnan Behlulovic humwambii kitu kwa Yanga
Adnan Behlulovic humwambii kitu kwa Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Novemba 04 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Novemba 04 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kazini kwa Kibwana bado kuna kazi
Kazini kwa Kibwana bado kuna kazi
18h ago
READ MORE β†’
Shalulile atabiriwa makubwa msimu huu
Shalulile atabiriwa makubwa msimu huu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga kurudi New Amaan Complex makundi CAFCL?
Yanga kurudi New Amaan Complex makundi CAFCL?
1d ago
READ MORE β†’
Nyota tisa wa Yanga kwenye majukumu ya timu za Taifa
Nyota tisa wa Yanga kwenye majukumu ya timu za Taifa
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 03 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 03 2026
1d ago
READ MORE β†’
Pacome aongeza matumaini ya kurejea mapema
Pacome aongeza matumaini ya kurejea mapema
1d ago
READ MORE β†’
Kwa Toure hapa Yanga imepata mshambuliaji
Kwa Toure hapa Yanga imepata mshambuliaji
2d ago
READ MORE β†’