Fundi Duke Abuya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Dec 2024
Fundi Duke Abuya

Baada ya kukosekana kiungo Khalid Aucho kutokana na majeraha, Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic amemtumia kiungo kiraka Duke Abuya katika majukumu yake

Ramovic alianza kumtumia Abuya katika eneo la kiungo cha ulinzi katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal na jana akamtumia katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc

Kiwango bora alichoonyesha Abuya katika mchezo huo, kilimfanya aondoke na tuzo ya nyota wa mchezo

Ni Abuya aliyeanzisha shambulizi lililozaa bao la pili baada ya pasi yake 'rula' kwa Clatous Chama, aliyemtengeneza Pacome kufunga bao hilo

Abuya amedhihirisha yuko tayari kwa majukumu yoyote ndani ya Yanga kwani hata Dickson Job alipoumia, alirudi nyuma kucheza eneo la beki wa kati

Ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namaungo Fc jana umeihakikishia Yanga kusogeza nafasi ya pili ikiwa na alama 27 sawa na Azam Fc timu hizo zikiwa na takwimu sawa ya mabao ya kufunga(16) na kufungwa (4)

Yanga iko nyuma ya Simba kwa tofauti ya alama 1 tu, Wananchi wamerejea rasmi katika kampeni ya kutetea ubingwa wao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumatano, Novemba 04 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Novemba 04 2026
2h ago
READ MORE β†’
Kazini kwa Kibwana bado kuna kazi
Kazini kwa Kibwana bado kuna kazi
15h ago
READ MORE β†’
Shalulile atabiriwa makubwa msimu huu
Shalulile atabiriwa makubwa msimu huu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga kurudi New Amaan Complex makundi CAFCL?
Yanga kurudi New Amaan Complex makundi CAFCL?
23h ago
READ MORE β†’
Nyota tisa wa Yanga kwenye majukumu ya timu za Taifa
Nyota tisa wa Yanga kwenye majukumu ya timu za Taifa
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 03 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 03 2026
1d ago
READ MORE β†’
Pacome aongeza matumaini ya kurejea mapema
Pacome aongeza matumaini ya kurejea mapema
1d ago
READ MORE β†’
Kwa Toure hapa Yanga imepata mshambuliaji
Kwa Toure hapa Yanga imepata mshambuliaji
1d ago
READ MORE β†’
Kangwanda ana kazi ya kufanya Yanga
Kangwanda ana kazi ya kufanya Yanga
2d ago
READ MORE β†’
Kocha tayari amewasili tutamtambulisha wakati wowote - Kamwe
Kocha tayari amewasili tutamtambulisha wakati wowote - Kamwe
2d ago
READ MORE β†’