Simba na Yanga kumaliza ubishi uwanja wa Taifa leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Apr 2018
Simba na Yanga kumaliza ubishi uwanja wa Taifa leo
Hatimaye siku imetimia kwa wakongwe wa soka nchini Simba na Yanga kushuka dimba la Taifa leo kuonyeshana kazi kwenye mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya ule wa awali kutoka sare ya bao 1-1.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza, ambao Yanga ilikuwa mwenyeji, ililazimisha sare baada ya kutokea nyuma na kusawazisha bao la Shiza Kichuya kupitia kwa Obrey Chirwa.

Mchezo wa leo unavuta hisia za mashabiki wa soka hususan kwa klabu hizo mbili zinazodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa, ambazo ndizo pekee zinazoonekana kuchuana katika mbio za kuwania ubingwa msimu huu.

Kuelekea mchezo huo wa leo, Kocha wa Simba, Pierre Lechantre, amesema akili zao wamezielekeza kwenye pointi tatu muhimu na si vinginevyo.

Kocha huyo Mfaransa, amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo huo na kila mchezaji amekuwa katika morali ya juu.

"Nataka kuona timu inacheza soka lake la kasi na kujitahidi kumaliza mchezo mapema, mabao ya mapema yatapunguza presha kwetu," alisema Lechantre.

Kauli hiyo iliungwa mkono na nahodha wa Wekundu wa Msimbazi hao, John Bocco, ambaye amesema wamejipanga kikamilifu na hawatapunguza kasi yao.

Kwa upande wake, kocha mpya wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema anaiheshimu Simba na ameona ina kikosi kizuri baada ya kufuatilia michezo yao, lakini hilo halimpi hofu kwa kuwa ana mbinu nyingi za kuwasimamisha vinara hao wa Ligi Kuu Bara.

"Sijakaa muda mrefu hapa, lakini nimekuja kipindi ambacho maandalizi ya mchezo yalikuwa yameanza, nimejaribu kuwafuatilia na imenisaidia kujua nini cha kufanya kuhakikisha tunapata ushindi," alisema Zahera.

Alisema amefahamu nguvu ya wapinzani wao ipo wapi na tayari wamefanyia kazi kuhakikisha wanapambana na kutoka na ushindi.

Nahodha wa Wanajangwani hao, Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema kuwa mchezo wa Simba na Yanga huwa hautabiriki.

Nadir amesema wanawaheshimu Simba kwa kuwa msimu huu wameonekana kuimarika, lakini hilo kwao haliwapi shida kwa kuwa wataingia uwanjani kupambana bila kujali wanacheza na nani.

"Siku zote mechi za Simba na Yanga ni ngumu na hazitabiriki, tunashukuru tupo vizuri kama wachezaji na tunaahidi kupambana kwa dakika 90 kuhakikisha tunaondoka na ushindi," alisema Cannavaro.

Endapo Yanga itafanikiwa kupata ushindi itakuwa imepunguza wingo wa pointi dhidi ya Simba ambayo ipo kileleni kwa pointi 11 zaidi licha ya Wanajangwani hao kuwa nyuma kwa mechi mbili.

Simba kwa upande wao ushindi utawafanya kuongeza wigo wa pointi, hivyo kuukaribia ubingwa msimu huu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’