Tusikubali kupoteza malengo yetu - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Nov 2024
Tusikubali kupoteza malengo yetu - Kamwe

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema nyakati ngumu ambazo wanapita sasa ni sehemu ya maisha katika mpira wa miguu

Hata hivyo Kamwe amesisitiza Yanga inapitia kipindi kigumu tu lakini bado haijapoteza malengo yake ya msimu

Jambo muhimu sasa ni kuhakikisha timu inabaki katika malengo, zaidi ni Mwananchi kuendelea kuwa wamoja ili kuhakikisha wanatoka salama katika kipindi hiki

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Kamwe ameandika ujumbe huu;

"Ndio maisha ya Football yalivyo. Ziko nyakati nzuri sana, utashinda na kufurahi kila unapokwenda uwanjani, kisha zitakuja nyakati ngumu"

"Utaipoteza kabisa furaha. Wachezaji watavuja jasho na bado matokeo hayatakuwa upande wako. That's Football. Yanga kwa sasa tuko kwenye hiki kipindi kigumu"

"Nini yatupasa kufanya kwa sasa? Kwanza kumshukuru M/Mungu. Ni yeye aliyetujaalia Neema nyakati za nyuma na Ni yeye anayetupitisha kwenye changamoto hivi sasa"

"Jambo la pili, Tuamini kuwa hiki ni kipindi kibaya Lakini BADO HATUNA MSIMU MBAYA. Tuna mechi 5 mbele za kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Na wapinzani wetu wengine jana wamepata sare na Tuna mechi nao 2, hivyo Nafasi Bado ipo wazi"

"Kwenye Ligi, Tofauti ni Pointi 4, na Tuna mechi mkononi, Nafasi ya kugeuza mambo iko wazi na ni kubwa mno. Na kama hivyo ndivyo, pamoja na maumivu yote tunayoyapitia hivi sasa Tusikubali kabisa kupoteza Focus yetu"

"Nyakati hizi yatasemwa mengi sana, muhimu kwetu ni kuwa makini na masikio yetu. Tusikilize, yale ya msingi tuyafanyie kazi, na yale ya kipuuzi, tuyapuuze"

"Hii inaweza kuwa nafasi ya adui zetu kutuvuruga zaidi ili tutoke relini. TUSIKUBALI. Bado Tuko katikati kwenye uwanja wa vita, Tupambane kwa ajili ya Yanga yetu"

"Focus yetu kwa sasa ni mechi ya Jumamosi Vs Namungo. Pointi hizi 3 ni muhimu sana kwenye Ligi ili kutoongeza gape kati yetu na wapinzani wetu"

"Muda ni mdogo sana kutoka sasa kwenda kwenye hii mechi, Tuwe watulivu Wananchi, Tuandae silaha zetu na In shaa Allah Twende Ruangwa tukaipambanie Yanga yetu"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yanga vs Kagera Sugar ni Jumapili hii, hivi hapa viingilio
Yanga vs Kagera Sugar ni Jumapili hii, hivi hapa viingilio
2h ago
READ MORE β†’
Nini matarajio urejeo wa pili wa Ramovic?
Nini matarajio urejeo wa pili wa Ramovic?
4h ago
READ MORE β†’
Kapteni Beka mbioni kurejea kikosini
Kapteni Beka mbioni kurejea kikosini
5h ago
READ MORE β†’
Kituo kinachofuata ni Kagera Sugar
Kituo kinachofuata ni Kagera Sugar
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
11h ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
23h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1d ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1d ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1d ago
READ MORE β†’