Miaka 36 imepita tangu Rashid Hanzuruni alipofunga bao wakati Simba na Yanga zilipokutana kwa mara ya kwanza Aprili 29, 1982, katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Hanzuruni alifunga bao dakika 2, na kuipa Yanga ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba, ikiwa ni mara ya kwanza na kesho itakuwa ni mara ya pili kwa timu hizo kukutana tarehe hiyo.
Pamoja na Yanga kupata ushindi katika mchezo huo wa kwanza bado rekodi zinaonyesha timu hizo zimekutana mara tisa mwezi Aprili katika michezo ya Ligi Kuu Bara huku sare zikiwa nne, Simba ikishinda mara tatu na Yanga ikishinda mara mbili.
Mechi iliyozalisha mabao mengi katika mwezi huu ni ile iliyofanyika Aprili 18, 2010 ambapo Simba iliichapa Yanga mabao 4-3.
Mabao ya Simba siku hiyo yalifungwa na Mussa Hassan Mgosi aliyefunga mawili, Uhuru Seleman na Hillay Echesa wakati mabao ya Yanga yalipachikwa wavuni ni Jerryson Tegege aliyefunga mawili na Athuman Iddi 'Chuji'.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE