Yanga ya Ramovic ni kushambulia mwanzo, mwisho

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Nov 2024
Yanga ya Ramovic ni kushambulia mwanzo, mwisho

Leo Yanga itakamilisha maandalizi kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal utakaopigwa kesho Jumanne katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Baada ya kuondoka Miguel Gamondi, shauku ya mashabiki wa Yanga ni kuona timu yao itacheza soka la aina gani chini ya kocha mpya, Mjerumani Sead Ramovic

Ramovic amewahakikishia mashabiki wa Yanga kuwa watarajie soka la kasi yaani kushambulia na kukaba pasipo kuwapa wapinzani nafasi ya kupumua

Katika mazoezi ya kikosi chake, Ramovic ameonekana kuwaelekeza vijana wake soka la kasi zikipigwa pasi za haraka kwenda mbele na mara kwa mara akiwataka kutumia nafasi wanazopata, lakini amekuwa akiwasisitiza kuutafuta mpira haraka sana wanapoupoteza.

Ramovic ameweka wazi falsafa ya soka lake hataki kuona mpinzani anapumua sawasawa akitaka kuona wachezaji wake wanashambulia kwa nguvu kwa wakati wote huku wakiwa na nidhamu ya kukaba.

"Aina hii ya soka inahitaji utimamu mkubwa wa mwili kwa wachezaji wetu na itahitaji muda, lakini naamini muda ukifika huko mbele tukiiva kwenye hili itawaimarisha wachezaji wetu mmoja mmoja na timu itakuwa kwenye ubora mkubwa"

"Kwa sasa tunachotaka ni kucheza kwa kasi, kuwasumbua wapinzani wasiwe na muda wa kupumua kujiuliza wamekosea wapi,"Β  Ramovic alinukuliwa na Mwanaspoti

"Unajua unaweza kwenda gym leo ukanyanyua vyuma lakini huwezi siku inayofuata ukawa umeshafanikiwa kutunisha misuli, lakini kuna hali ya utofauti ya mwili utaisikia na hiki ndicho tunakifanya sasa"

"Kuna baadhi ya vitu tunaweza kuviona vinaanza kubadilika lakini tunapotaka tutahitaji muda, tukifanikiwa tunachofanya sasa hakika matokeo yetu yatakuwa mazuri," alisema Ramovic

Ramovic ametua Yanga akitokea klabu ya TS Galaxy ya Afrika Kusini ambayo msimu uliopita aliingoza kumaliza nafasi ya sita katika msimamo wa ligi hiyo

Msimu huu Ramovic aliiongoza Galaxy katika mechi sita tu kabla ya kuachia ngazi baada ya kutofurahishwa na kitendo cha wamiliki wa timu hiyo kuuza nyota tegemeo na kupelekea timu hiyo kupoteza makali yake

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21m ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
39m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
45m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’