Katika wachezaji 13 wa Yanga ambao wameshiriki kampeni ya kuwania kufuzu fainali za Afcon 2025, wakiwa na timu zao za Taifa, 12 wamesaidia Mataifa yao kufuzu kwa michuano hiyo
Yaani unaweza kusema zaidi ya wachezaji 10 wa Yanga wanaweza kukutana Morocco mwakani katika fainali za michuano hiyo
Djigui Diarra amefuzu akiwa na Mali, Ibrahim Bacca, Dickson Job, Mudathir Yahya, Clement Mzize, (Bakari Mwamnyeto na Nickson Kibabage waliitwa mechi zilizopita) wote wameshiriki kuhakikisha Tanzania inafuzu kwa mara ya nne katika michuano hiyo
Khalid Aucho ameiongoza Zambia kufuzu kwa michuano hiyo huku Stephane Aziz Ki akiwa sehemu ya kikosi cha Burkina Faso kilichokata tiketi mapema kufuzu kwa michuano hiyo
Kennedy Musonda na Clatous Chama wao walikuwa sehemu ya kikosi cha Zambia kilichofuzu Musonda akiwa kinara wa mabao katika kikosi hicho akipachika mabao manne
Princee Dube pia alikuwa sehemu ya kikosi cha Zimbabwe kilichofuzu kwa michuano hiyo akipachika bao moja
Ni Duke Abuya pekee ambaye timu yake ya Taifa ya Kenya haikupata nafasi ya kufuzu lakini alikuwa na mchango mkubwa katika kikosi cha Harambee Stars
Tutarajie Afcon 2025 kuwa na mastaa kibao kutoka klabu ya Yanga...!