Ni takribani wiki moja imebaki kuelekea mchezo wa kwanza hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika kati ya Yanga dhidi ya Al Hilal
Novemba 26 Wananchi watakuwa na kazi moja tu, kusaka ushindi mbele ya Al Hilal katika mechi ya kisasi itakayopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, saa 10 jioni
Mauzo ya tiketi kuelekea mchezo huo yameanza mapema ili kuwapa nafasi mashabiki wa Yanga kununua tiketi zao mapema na kuhakikisha wanaujaza uwanja wa Benjamin Mkapa
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewaasa Wananchi kununua tiketi mapema ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza katika siku za mwisho kuelekea mchezo huo
Viingilio ni rafiki sana, kwa Tsh 3,000/- unaweza kushuhudia mchezo huku ukiwaongezea hamasa vijana wa kocha Sead Ramovic ambaye tayari yuko mitamboni kuandaa timu ya ushindi