Wachezaji Yanga waahidi makubwa Ligi ya Mabingwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Nov 2024
Wachezaji Yanga waahidi makubwa Ligi ya Mabingwa

Nahodha wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto amesema wachezaji wana jukumu kubwa la kupambana katika michuano ya ligi ya mabingwa ili kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi ya mafanikio waliyopata msimu uliopita

Kikosi cha Yanga kilirejea mazoezini juzi kuanza maandalizi ya mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya Al Hilal utakaopigwa Jumanne Novemba 26 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Mwamnyeto amesema wachezaji wamerejea wakiwa na ari kubwa focus yao ikiwa ni mchezo dhidi ya Al Hilal

"Tunashukuru wachezaji wote tumerejea mazoezini tukiwa salama, focus yetu tumeielekeza kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal"

"Msimu huu tuna jukumu kubwa la kuhakikisha tunafanya vizuri zaidi katika michuano hii kuvuka hatua hii ya makundi na kucheza robo fainali"

"Tuna muda mzuri wa kujiandaa na mchezo dhidi ya Al Hilal naamini wenzetu waliokwenda katika majukumu ya timu za Taifa watakaporudi kuungana nasi tutakuwa tayari kwa mchi hiyo," alisema

Yanga iko kundi A ikiwa pamoja na Al Hilal, TP Mazembe na MC Alger. Baada ya mchezo wa nyumbani dhidi ya Al Hilal, Wananchi watasafiri ugenini Algeria kuikabili MC Alger Disemba 07

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yanga yaweka nguvu kufuzu hatua ya makundi CAFCL
Yanga yaweka nguvu kufuzu hatua ya makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mwenda arejeshwa rasmi kikosini Yanga
Mwenda arejeshwa rasmi kikosini Yanga
12h ago
READ MORE β†’
Abuya nje wiki mbili
Abuya nje wiki mbili
12h ago
READ MORE β†’
Malengo yetu mbio za ubingwa Ligi Kuu yako palepale - Kamwe
Malengo yetu mbio za ubingwa Ligi Kuu yako palepale - Kamwe
12h ago
READ MORE β†’
Manqoba apewa mtihani Ligi ya Mabingwa
Manqoba apewa mtihani Ligi ya Mabingwa
14h ago
READ MORE β†’
Yao awaangukia mashabiki Yanga 'Tutakuwa bora zaidi'
Yao awaangukia mashabiki Yanga 'Tutakuwa bora zaidi'
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 13 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 13 2026
18h ago
READ MORE β†’
Aucho atangaza kustaafu timu ya Taifa Uganda
Aucho atangaza kustaafu timu ya Taifa Uganda
1d ago
READ MORE β†’
Tusubiri kamati ya saa 72 itaamua nini tukio hili
Tusubiri kamati ya saa 72 itaamua nini tukio hili
1d ago
READ MORE β†’
TRA United vs Yanga kupigwa Oktoba 24
TRA United vs Yanga kupigwa Oktoba 24
1d ago
READ MORE β†’