Licha ya Yanga kukanusha kumuajiri aliyekuwa Kocha Mkuu wa KMC, Abdihamid Moallin, unaweza kusema ni suala la muda tu Moallin atatua kwa Wananchi
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa KMC, zimethibitisha kuwa Moallin ameondoka na mwenyewe akiweka bayana kujiunga na Yanga
Aidha Yanga italazimika kumaliza na KMC kabla ya kumtangaza Moallin kwa sababu bado alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa klabu ya KMC FC, Songoro Mnyonge, amethibitisha Moallin kuelekea Jangwani huku akiitaka Yanga kutimiza taratibu za kuvunja mkataba wa kocha huyo aliyeitumikia KMC kwa msimu mmoja
Licha ya kuwa na leseni ya ukocha, Moallin ni 'Video Analyst' na pengine Yanga inaweza kumuajiri katika nafasi hiyo kama sio kocha msaidizi kama alivyokanusha msemaji wa Yanga Ali Kamwe mapema leo