Gamondi ahakikishiwa uungwaji mkono

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Nov 2024
Gamondi ahakikishiwa uungwaji mkono

Mkufunzi wa Yanga Miguel Gamondi anaungwa mkono na uongozi kwa asilimia 100 na amepewa baraka zote kukiandaa kikosi chake kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal ya Sudan, utakaochezwa Novemba 26, mwaka huu, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Klabu hiyo, Alex Ngai, amesema kuwa tetesi za kwamba klabu hiyo itamtimua Gamondi na kumleta kocha mwingine hazina ukweli wowote na kuwataka wanachama na mashabiki wa timu hiyo kutokuwa na wasiwasi wowote kwani viongozi wa Yanga bado wana ushirikiano na benchi la ufundi

"Yanazungumzwa mengi, lakini niwahakikishie wanachama, mashabiki wa Yanga kuwa viongozi wote wa Yanga wapo vizuri, tuna ushirikiano na benchi la ufundi, tutakaa na kufanya tathmini na tunaendelea na maandalizi ya mechi yetu dhidi ya Al Hilal ya Sudan, mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Fountain Gate tuliokuwa tucheze Novemba 21 imeshaondolewa kwenye ratiba," alisema Ngai

Ngai amesema pamoja na ukweli kwamba kuondolewa kwa kocha kwenye timu yoyote ile si jambo la ajabu, lakini kwa Yanga haiwezi kuwa hivi sasa kwani hakuna mpango huo kama inavyoelezwa

"Kwa kweli siwezi kusema kama ni kweli, haina ukweli, Yanga ni timu kubwa, niwaondoe hofu tuko kwenye maandalizi, kama lolote litatokea basi haitokuwa ajabu lakini kwa sasa sitarajii kitu kama hicho.Tunamsapoti, na tutaendelea kumpa sapoti," alisema

Akizungumzia vipigo viwili mfululizo ambavyo timu hiyo imevipata kutoka kwa Azam FC na Tabora United, Ngai alisema ni hali ya mchezo na watakaa sawa na kurekebisha mambo kabla ya kurejea tena kwenye reli

"Sidhani kama tunapitia kipindi kigumu, ni hali tu ya mchezo, katika mpira wa miguu vitu kama hivi huwa vinatokea, bahati mbaya sana tumepoteza mechi mbili mfululizo, mfano kwenye mchezo dhidi ya Tabora, safu yetu yote ya ulinzi haikuwapo, wengine walikuwa na kadi za njano, wengine wamesimamishwa na baadhi majeruhi pia, hali ile ilituathiri sana mpaka ikafikia Khalid Aucho akarudishwa nyuma kwenda kucheza nafasi ya beki, hii ni changamoto tu tutarudi kwenye reli kama kawaida," alisema

Katika mchezo dhidi ya Tabora United, Yanga iliwakosa Yao Kouassi ambaye ni majeruhi, Ibrahim Hamad 'Bacca' aliyekuwa akitumikia adhabu ya kadi nyekundu na Dickson Job aliyekuwa na kadi tatu za njano

Ngai amesisitiza pamoja na kupoteza, Yanga bado iko kwenye mbio za ubingwa na ni moja kati ya timu zinazojua kuchanga karata zake kuelekea kwenye mbio hizo, hivyo kuwataka mashabiki kutokata tamaa badala yake kuendelea kuisapoti

"Yanga ni moja kati ya timu zinazojua kuchanga karata zake kuelekea kwenye ubingwa wa Tanzania Bara kwa hiyo hii wala haitusumbui, imeshatokea imeshapita, ninachowaomba wanachama na mashabiki waendelee kuisapoti timu yao," alisema

IPP Media

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kuumia kwa Abuya kulitugharimu - Manqoba
Kuumia kwa Abuya kulitugharimu - Manqoba
32m ago
READ MORE β†’
Mchezo dhidi ya TRA United kupangiwa tarehe nyingine
Mchezo dhidi ya TRA United kupangiwa tarehe nyingine
52m ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 2-1 Yanga, Ligi Kuu (FT)
Highlights; Simba 2-1 Yanga, Ligi Kuu (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumapili, Oktoba 11 2026
Magazeti ya leo Jumapili, Oktoba 11 2026
2h ago
READ MORE β†’
Simba walikuwa bora, Yanga wameonyesha uchovu
Simba walikuwa bora, Yanga wameonyesha uchovu
10h ago
READ MORE β†’
Bado tuna mechi 23 msimu huu - Kamwe
Bado tuna mechi 23 msimu huu - Kamwe
10h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 2-1 Yanga, NBC PL
FT : Simba 2-1 Yanga, NBC PL
12h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs Yanga, NBC PL, Oct 10
Kikosi : Simba vs Yanga, NBC PL, Oct 10
15h ago
READ MORE β†’
Boka, Yao tayari kwa kazi maalum dabi ya Kariakoo
Boka, Yao tayari kwa kazi maalum dabi ya Kariakoo
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Simba vs Yanga, NBC PL, Oct 10
Matchday; Simba vs Yanga, NBC PL, Oct 10
23h ago
READ MORE β†’