Baada ya mapumziko ya mwishoni mwa wiki, kikosi cha Yanga leo kinarejea mazoezini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal ambao utapigwa Novemba 26 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema timu itaanza na program ya mazoezi ya Gym majira ya saa 6 mchana
"Focus yetu kwa sasa tumeielekeza kwenye ligi ya mabingwa mchezo dhidi ya Al Hilal ambao utachezwa Novemba 26 katika uwanja wa Benjamin Mkapa"
"Timu inarejea mazoezini leo ambapo mchana tutakuwa na 'session' ya Gym pale Gymkhana"
"Tunakwenda kujiandaa kikamilifu kuelekea mchezo dhidi ya Al Hilal, mchezo huu tunautaka kwelikweli," alisema Kamwe
Katika hatua nyingine, Kamwe amewataka wale wenye maswali kuhusu kocha Miguel Gamondi wafike Gymkhana na maswali yao waliyoyaandaa kwa lugha ya kiingereza kwani atakuwa tayari kujibu maswali yote
"Nimewaambia wanahabari wanaouliza kuhusu Master Gamondi wafike Gymkhana na maswali yao yaliyo katika lugha ya kiingereza, atawajibu wote," alisema
Gamondi anaendelea na majukumu yake ya kukinoa kikosi cha Yanga licha ya taarifa za mitandaoni na baadhi ya magazeti kudai ameondolewa katika nafasi yake